Wednesday, February 13, 2013
SOKA HAWAFANYI JITIHADA ZA KUTOSHA KUPAMBANA NA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.
RAIS wa Shirika la Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu Duniani-WADA, John Fahey amesema kuwa mamlaka za mchezo wa soka bado hazijafanyi vipimo vya damu vya kutosha ili kupambana na wachezaji wadanganyifu. Akizungumza na waandishi wa jijini London, Fahey amesema waau wa soka wanatakiwa kuongeza juhidu zaidi kupambana na suala la utumiaji dawa za kuongeza nguvu na shirika lake litafanya nao kazi bega kwa bega kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Rais huyo aliendelea kusema kuwa kwenye soka hakufanyiki vipimo vya damu vya kutosha iangwa uwezo wa kufanya hivyo wanao ambapo wanajaribu kuwashawishi kufanya vipimo hivyo zaidi ili kuhakikisha wanatokomeza kabisa vitendo hivyo michezoni. Fahey pia ameonyeshwa kusikitishwa kwake na mchezo wa soka kukataa kutumia mfumo wa pasi za kibaologia ikiwa kama sehemu ya kupambana na wachezaji wadanganyifu wanaotumia dawa hizo za kuongeza nguvu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment