Saturday, March 2, 2013

BLATTER KUANZISHA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA UBAGUZI.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema wanatarajia kuanzisha kikosi kazi kwa ajili kupambana tatizo la ubaguzi wa rangi katika soka. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Edinburgh kabla ya mkutano wa bodi unaotarajiwa kufanyika baadae leo, Blatter amesema kikosi kazi hicho kitaongozwa na rais wa Shirikisho la Soka kwa nchi za Amerika kaskazini na kati na Caribbean-Concacaf Jeffrey Webb. Kwa muda mrefu mchezo wa soka umekuwa ukitawaliwa na matukio ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki hususani sehemu za Ulaya mashariki pamoja na adhabu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa. Blatter amekiri kuwa ubaguzi ni tatizo kubwa katika mchezo wa soka ndio maana ameamua kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili kuangalia uwezekano wa kutokomeza mambo ya kibaguzi. Blatter pia atakutana na kiungo wa AC Milan Kevin-Prince Boateng baadae mwezi huu kujadili njia za kutumia kutokomeza ubaguzi baada ya mchezaji huyo kutengeneza vichwa vya habari kwa kuongoza wachezaji wenzake kutoka uwanjani baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi.

No comments:

Post a Comment