Sunday, March 10, 2013

GAZZA AREJEA UINGEREZA BAADA YA MATIBABU.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Paul Gascoigne aliyekuwa akijulikana zaidi kwa jina la Gazza amebainisha kuwa alifikiri angekufa baada ya dawa za kutibu tatizo la pombe alilonalo kumdhuru. Gazza mwenye umri wa miaka 45 alilazwa katika kliniki huko Phoenix, Arizona nchini Marekani baada ya kjitumbukiza kwa mara nyingine katika ulevu wa kupindukia ambao ulikuwa ukitishia maisha yake. Lakini wakati akiwa katika matibabu hayo baadhi ya dawa alizokuwa akipewa ili kumsaidia kuondokana na tatizo hilo zilimdhuru vibaya na kupelekea kukimbizwa hospitali na kuwekwa katika chumba chenye uangalizi maalumu. Mara baada ya kurejea nchini Uingereza kutoka katika matibabu yake nyota huyo amebainisha kuwa tatizo lilimpata lilikuwa kubwa na hata yeye mwenyewe hakudhani kama angeweza kuvuka kikwazo hicho. Gazza amesema madaktari watatu waliokuwa wakimtibu hawakuamini kama anaweza kuamka tena baada ya dawa hizo kumdhuru lakini anashukuru yuko salama na tukio hilo litakuwa kama changamoto kwake ili asiweze kurejea katika ulevi tena.

No comments:

Post a Comment