Friday, March 1, 2013

GFA LAWAANGUKIA WATOTO PELE.

SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA limewaangukia watoto wa nguli wa zamani wa soka wa nchi hiyo Abeid Ayew Pele likiwaomba kuangalia upya uamuzi wao wa kujitoa kwa muda kuchezea timu ya taifa. GFA iliwaandikia barua rasmi Andres na mdogo wake Jordan Ayew wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa ikiwaomba kubadilisha uamuzi huo na kujaribu kutatua matatizo waliyonayo kwa mazungumzo. Andres aliandika barua kwenda shirikisho hilo kulitaka kumuondoa katika kipango kwani ameamua kupumzika kwa muda kwasababu ya kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi huku mdogo wake akidai shirikisho hilo halithamini mchango wake katika timu ya taifa ya nchi hiyo. Wadau mbalimbali wa michezo nchini Ghana akiwemo rais wa zamani wa GFA Dr Nyaho Tamakloe walilitaka shirikisho hilo kukaa na vijana hao kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hilo kwa manufaa ya soka la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment