Thursday, March 14, 2013

IT'S A WAKE UP CALL FOR ENGLAND FOOTBALL - WENGER.

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa kukosekana kwa klabu za Uingereza katika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni somo kubwa kwa soka la nchi hiyo. Ushindi wa Bayern Munich ya Ujerumani kwa bao la ugenini dhidi ya Arsenal jana unamaanisha kuwa Uingereza haitakuwa na timu katika robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka msimu wa mwaka 1995-1996. Wenger amesema ni kitu kinachokatisha tamaa kwa soka la Uingereza kukubali nchi zingine Ulaya kuwapita wakati wamekuwa wakitamba katika michuano hiyo kwa kipindi cha miaka 17 mfululizo. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini humo Manchester City walimaliza wa mwisho katika hatua ya makundi yaliyoshirikisha timu za Real Madrid, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi zao sita walizocheza. Wakati mabingwa watetezi Chelsea ambao waliifunga Bayern katika fainali za mwaka jana nao pia walishindwa kupenya katika hatua ya makundi huku Manchester United wao walijikuta wakitolewa na Real Madrid katika hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment