Wednesday, March 13, 2013
MESSI ADHIHIRISHA UBORA WAKE.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amewatumia ujumbe watu waliokuwa wakidhani amekwisha kwa kupachika mabao mawili maridadi na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi mabao 4-0 katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan. Barcelona inakuwa timu ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kupindua matokeo ya mabao 2-0 waliyofungwa na Milan nchini Italia wiki tatu zilizopita na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 4-2. Messi ambaye ni mfungaji bora wa michuano hiyo kwa misimu minne iliyopita alikuwa akituhumiwa kushindwa kucheza katika kiwango cha juu katika mechi kubwa lakini katika mchezo wa jana dhidi ya Milan aliwanyamazisha midomo wale wote waliokuwa wakiamini hivyo. Bao la kwanza nyota huyo alifunga katika dakika tano ya mchezo na kuongeza lingine la pili dakika ya 40 huku mabao mengine yakifungwa na David Villa na Jordi Alba katika kipindi cha pili cha mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mpaka sasa amefunga mabao 53 kwenye mechi 42 alizocheza katika mashindano yote msimu huu huku 40 kati ya hayo akiwa amefunga katika La Liga na mengine saba katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment