
Monday, March 18, 2013
RIBERY AANZA MAZOEZI MEPESI.
WINGA machachari wa klabu ya Bayern Munich, Frank Ribery ameanza mazoezi binafsi tena baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na matatizo ya kuumia kifundo cha mguu. Mchezaji nyo wa kimataifa wa Ufaransa alipata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani dhidi ya Dusseldorf Machi 9 maumivu ambayo yalipelekea kuikosa mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal ambao walifungwa mabao 2-0 na mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen ambao walishinda mabao 2-1. Hatahivyo nyota huyo anaonekana kukaribia kupona baada ya kuanza mazoezi binafsi bila ya kuonyesha kuwa na tatizo lolote. Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps alidai mwishoni mwa wiki kuwa anategemea nyota huyo atakuwa fiti kwa wakati kabla ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Georgia Ijumaa na Hispania utakaochezwa siku nne baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment