Tuesday, April 2, 2013

BECKHAM ATAMANI KUITUMIKIA UINGEREZA.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham amesema bado ana matumaini ya kuichezea nchi yake katika siku za usoni. Akihojiwa na kituo cha CNN kiungo huyo ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Paris saint-Grmain-PSG ya Ufaransa amesema anajua amekaribia kufikisha umi wa miaka 38 hivyo nafasi yake ya kuitwa ni ndogo lakini amedai huwezi kujua nini kitatokea huko mbele. Beckham ni mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Uingereza lakini hajaitwa na timu hiyo toka Octoba mwaka 2009. Nyota huyo amesema mojawapo ya vitu vinavyomfanya asistaafu kucheza soka la kimataifa ni kwasababu kama nafasi itatokea ya kuitwa tena yeye atakuwa tayari. Kiungo huyo amejumuishwa katika kikosi cha PSG ambacho kitakuwa na kibarua kizito kwa kuikaribisha Barcelona katika mchezo wa kwanza robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment