Saturday, April 13, 2013

MARADONA ATEMBELEA KABURI LA RAFIKI YAKE CHAVEZ.

NGULI wa soka wa Argentina, Diego Maradona ametembelea kaburi la rafiki yake Hugo Chavez Ijumaa na kuwataka wananchi wa Venezuela kumchagua mteule wa Chavez katika uchaguzi wa rais. Akiwa amevalia shati jeupe na hereni za almasi katika kila sikio lake, Maradona aliwaomba wananchi wa Venezuela kumchagua Nicolas Maduro ili kumuenzi Chavez aliyekuwa akihusudu siasa za kijamaa. Maradona amesema wananchi hao wanatakiwa kuendelea na mapambano kwani pamoja na kwamba hawako na rais wao kipenzi Chavez lakini wanaweza kumchagua Maduro ili kuendelea yale yote mazuri aliyokuwa akiyafanya. Nguli huyo alihudhuria kampeni za mwisho za Maduri zilizofanyika jijini Caracas Alhamisi iliyopita na kutia saini mipira kadhaa kabla ya kuipiga kuelekea kwa wananchi waliokuja kusikiliza kampeni hizo. Maradona pia aliomba radhi kwa familia ya Chavez kwa kushindwa kuhudhuria mazishi ya rafiki yake huyo kipenzi yaliyofanyika Machi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment