Monday, April 1, 2013

MURRAY AKWEA MPAKA KATIKA NAFASI YA PILI KWA UBORA DUNIANI.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kumfunga David Ferrer wa Hispania na kunyakuwa taji la michuano ya wazi ya Sony iliyokuwa ikifanyika jijini Miami, Florida nchini Marekani. Katika mchezo huo Murray alimfunga Ferrer kwa 2-6 6-4 7-6 ushindi ambapo pia umempandisha mpaka katika nafasi ya pili katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Murray ambaye hilo ni taji lake la pili alikiri kuwa ulikuwa mchezo mgumu na yoyote kati yao angeshinda kwasababu wote walikuwa wamechoka katika dakika za mwishoni. Mara ya mwisho Murray ambay yuko nyuma Novak Djokovic anayeshika namba moja katika orodha hizo, kushika nafasi ya pili ilikuwa ni mwaka 2009 wakati Roger Federer akiwa namba moja.

No comments:

Post a Comment