
Monday, April 8, 2013
USAJILI NDIO ULIOTUANGUSHA - MANCINI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini anaamini kuwa klabu hiyo ingeweza kuwemo katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza na Ligi ya Mabingwa Ulaya kama wangefanya usajili mzuri msimu uliopita. Mancini alikuwa akiwahitaji wachezaji Robin van Persie, Eden Hazard, Daniele De Rossi na Javi Martinez ili kuongeza nguvu katika kikosi chake. Lakini aliwakosa wote hao na badala yake aliwasajili Jack Rodwell, Javi Garcia, Scott Sinclair, Matija Nastasic na Maicon. Kati ya wachezaji wote hao ambao City ilisajili ni mchezaji mmoja tu Nastasic ndio amekuwa na mafanikio toka atue kwenye klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezi wa ligi wakiwa nyuma kwa alama 15 mbele ya vinara Manchester United. City wanakabiliwa na kibarua kigumu baadae leo wakati watakapopambana na Manchester United katika Uwanja wa Old Traford katika mchezo wa ligi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment