Tuesday, May 14, 2013
BLATTER APONDA ADHABU WALIYOPEWA AS ROMA KWA UBAGUZI.
RAIS wa Shirikisho ka Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ameponda adhabu ya faini ya kiasi cha euro 50,000 waliyopewa klabu ya AS Roma ya Italia kwa tabia za kibaguzi walizoonyesha mashabiki wake akidai kuwa ni ndogo na haikubaliki. Blatter amesema atazungumza na Shirikisho la Soka la Italia ambalo amedai kuwa hawakufanya uchunguzi wa kutusha kuhusiana na tukio hilo la lililotokea Jumapili iliyopita katika katika mchezo kati ya AC Milan na Roma kwenye Uwanja wa San Siro. Blatter aliuambia mtandao wa FIFA kuwa ameshangazwa na kushindwa kuelewa kwanini kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka la nchi hiyo itoe maamuzi wa kuwatoza faini Roma kwa kipindi kifupi namna hiyo bila kuchunguza tukio kwa undani. Amesema kiwango walichotozwa Roma ni kidogo sana ukilinganisha ukubwa wa tatizo lenyewe ndio maana anataka kuzungumza na shirikisho hilo kuwatahadharisha kuwa njia waliyotumia sio sahihi kama wanataka kutokomeza tatizo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment