Friday, May 3, 2013

BLATTER KUOGOMBEA TENA FIFA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ametoa dondoo ya kwamba ana mpango wa kugombea tena nafasi hiyo kwa miaka minne mingine wakati wa hotuba yake mara baada ya mkutano na viongozi wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC nchini Malaysia. Mapema Machi mwaka huu Blatter amesema ana mpango kwa kuachia ngazi wakati atakapomaliza kipindi chake cha miaka minne kitakapoisha mwaka 2015 lakini akaongeza kuwa ataachia nafasi hiyo pale atakapoamini kwamba atakayemwachia anaweza kulisongesha mbele gurudumu la shirikisho hilo. Blatter mwenye umri wa miaka 77 alirudia tena kauli ya katika mkutano wa AFC jijini Kuala Lumpur jana akidai kuwa yeye ni nahodha na hawezi kuachia meli yake izame wakati bado anaona ana nguvu za kuizuia isifanye hivyo. Kauli hiyo ya Blatter imewafanya wachambuzi wa mambo ya soka wadai kuwa rais huyo ana mpango wa kugombea urais kwa kipindi kingine baada ya kumaliza hiki cha sasa mwaka 2015. Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini ambaye alikuwepo katika mkutano huo ambao ulishuhudia Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain akiteuliwa kuwa rais wa AFC, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kushika nafasi ya Blatter atakapoacia madaraka.

No comments:

Post a Comment