Thursday, May 9, 2013

ETO'O AIWEZESHA ANZHI KUTINGA FAINALI KOMBE LA URUSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Samuel Eto’o ameiwezesha klabu yake hiyo kutinga hatua fainali ya Kombe la Urusi jana. Bao pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon alilofunga katika dakika ya 61 lilitosha kuwazamisha wapinzani wao timu ya Zenit Saint Petersburg katika mchezo huo wa nusu fainali. Pamoja na Zenit kufanikiwa kumiliki sehemu kubwa ya mchezo huo lakini walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata hivyo kuwapa nafasi vijana wa Anzhi wanaonolewa na Guus Hiddink kuibuka kidedea. Anzhi sasa wanatarajiwa kucheza na CSKA Moscow katika mchezo wa fainali baada ya timu hiyo nayo kufanikiwa kuifunga Rostov kwa mabao 2-0 katika nusu fainali nyingine iliyofanyika Juzi. Fainali itachezwa Juni mosi mwaka huu katika huko jijini Grozny, Chechnya.

No comments:

Post a Comment