
Wednesday, May 8, 2013
GERRARD KUFANYIWA UPASUAJI WA BEGA.
NAHODHA wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bega baadae wiki hii upasuaji ambao utamuweka nje katika mechi mbili za klabu hiyo zilizobakia. Gerrard ambaye amekuwa na mchango katika kikosi chake msimu huu kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mchezo wa kirafiki katika Uingereza dhidi ya Ireland katika Uwanja wa Wembley na ule wa ugenini dhidi ya Brazil unaotarajiwa kuchezwa June 2. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa maumivu ya bega ya Gerrard yamekuwa yakiongezeka katika wiki za karibuni na kumhitaji kufanyiwa upasuaji wa lazima ili kutibu tatizo hilo. Klabu hiyo imesema wanatarajia kiungo huyo atakuwa amepona mapema wakati wa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment