Tuesday, May 21, 2013
MICHO KUINOA THE CRANES.
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic Micho anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya timu ya taifa Uganda inayojulikana kama The Cranes. Micho ambaye ni raia wa Serbia anatarajiwa kutangazwa mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Uganda-FUFA na kumaliza tetesi zilizozagaa karibu mwezi mzima baada ya kutimuliwa kwa Bobby Williamson mwezi uliopita. Micho mwenye umri wa miaka 43 alitimuliwa kuinoa Rwanda mwezi huohuo ambao Bobby naye alitimuliwa kuifundisha The Cranes na sababu za kutimuliwa kwao zinafanana kwani wote wawili timu zao zilikuwa zikifanya vibaya katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Changamoto ya kwanza atakayokutana nayo Micho ni kukirejesha kikosi hicho katika ari ya ushindani na kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zao za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia pamoja na ile ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani-CHAN.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment