Wednesday, May 22, 2013

MURRAY AJITOA FRENCH OPEN.

MCHEZAJI nyota wa tenisi kutoka Uingereza Andy Murray amejitoa katika michuano ya wazi ya Ufaransa kutokana na maumivu ya mgongo yaliyopelekea kushindwa kuendelea kucheza katika michuano ya wazi ya Italia. Murray ambaye anashika namba mbili katika orodha za ubora Duniani kwa upande wa wanaume amejitoa katika michuano hiyo baada ya kushauriwa na madaktari wake na anatarajia kurejea tena uwanjani katika michuano ya Wimbledon katikati ya mwezi ujao. Nyota huyo ambaye ni bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani amesema umekuwa ni uamuzi mgumu kufanya kwani huwa anapenda kucheza jijini Paris lakini imekuwa nje ya uwezo wake kwasababu ya ushauri wa kiafya aliopewa. Murray aliwaomba radhi waandaaji wa michuano hiyo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumtumia ujumbe wa kumuunga mkono na sasa kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kuhakikisha anapona na kurejea haraka uwanjani.

No comments:

Post a Comment