Friday, May 17, 2013
SHARAPOVA AJITOA ITALIAN OPEN.
MWANADADA nyota wa mchezo wa tenisi, Maria Sharapova amejitoa katika michuano ya wazi ya Italia kabla ya mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Sara Errani wa Italia kutokana na matatizo ya kimwili. Sharapova ambaye ni raia amejitoa mapema kwenye michuano hiyo ili aweze kupona haraka kwa ajili ya kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa baadae mwezi huu. Kwa upande mwingine mwanadada anayesshika namba moja katika orodha za ubora Serena Williams wa Marekani ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kumchakaza bila huruma Dominika Cibulkova wa Slovakia kwa 6-0 6-1 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Williams ambaye ameshinda mechi 21 mfululizo sasa atachuana na Carla Suarez Navarro wa Hispania kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment