Saturday, May 4, 2013

SIJAJUA HATMA YANGU - MANCINI.

MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amekiri kuwa bado hatapewa taarifa kama ataendelea kuinoa klabu hiyo msimu ujao. Baada ya kumaliza msimu bila ya mafanikio katika Ligi Kuu nchini UIngereza na Ligi ya Mabingwa Ulaya, kumekuwa na tetesi kuhusu mstakabali wa kocha huyo raia wa Italia huku wakala wa kocha wa Malaga ya Hispania Manuel Pellegrini akidaiwa kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa City, Txiki Begiristain. Mancini amesema hawajazumza chochote na mabosi wake kuhusu mustakabali wake ingawa amedai kuwa wana mawasiliano mazuri kwani ndani ya miaka miwili wameshinda mataji matatu na mwaka huu pia wana nafasi ya kushinda moja huku wakimaliza ligi katika nafasi ya pili. Baada ya hapo, Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak anaweza kuachukua uamuzi wowote kuhisiana na nafasi hiyo lakini kwasasa hana tatizo na kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment