Wednesday, May 1, 2013

TUNAPASWA KUHESHIMIWA - KLOPP.

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ametamba kuwa timu yake sasa inapaswa kutambulika kama mojawapo ya timu mahiri za soka barani Ulaya baada ya kuwabandua nje Real Madrid. Klopp ameongeza kuwa kwasas hawajali hawajali ni nani watakayekutana naye katika fainali, lakini kila mtu ataona kuwa hawatakwenda Wembley kama watalii bali kushinda kombe. Hata hivyo kocha huyo amemshutumu mwamuzi Howard Webb wa Uingereza akidai kuwa kuna matukio ambayo beki wa Madrid Sergio Ramos alistahili kupewa adhabu kali, kutokana na namna alivyokuwa akimchezea kimabavu Robert Lewandowski. Matokeo hayo ya Madrid yameendelea kuibua maswali kuhusiana na hatma ya Mourinho lakini mwenyewe amesema atasubiri hadi mwisho wa msimu ili kujadili na wasimamizi wa klabu kuhusu mkataba wake. Mourinho amesema anafahamu kuwa anapendwa nchini Uingereza, anapendwa na mashabiki na vyombo vya habari lakini hali ni tofauti nchini Hispania kwani ni wachache ndio wanaompenda.


No comments:

Post a Comment