Saturday, May 18, 2013

TUTAZUNGUMZIA MKATABA MPYA WA LOEW BAADA YA KUFUZU - BIERHOFF

MENEJA mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Oliver Bierhoff amesema mazungumzo kuhusu kumuongeza mkataba kocha wa timu hiyo Joachim Loew yataanza mapema timu hiyo itakapofuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Bierhoff alikaririwa na gazeti la Bild akisema kwamba watakaa pamoja na rais wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB Wolfgang Niersbach na katibu mkuu Helmut Sandrock mapema timu itakapokuwa imefuzu ili kuangalia uwezekano wa kumuongeza mkataba Loew. Mkataba wa Loew ambaye ameanza kuinoa Ujerumani toka mwaka 2006 na wasaidizi wake Hansi Flick na Andreas Koepke unamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kwasasa Ujerumani ndio wanaoongoza kundi lao na kama mambo yakienda vyema kikosi hicho cha Loew kinaweza kikakata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia Septemba mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment