Wednesday, May 22, 2013

UEFA YAWAONDOLEA ADHABU MALAGA.

KLABU ya Malaga ya Hispania inatarajia kushiriki michuano ya vilabu ya Ulaya msimu ujao baada ya Shirikisho la Soka barani humo-UEFA kutangaza kuwaondolewa adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja jana. Malaga ambayo ilitinga hatua ya ilitinga hatua ya robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu walifungiwa mwaka mmoja na UEFA kwa kukiuka utaratibu wa mambo ya fedha lakini walikata rufani katika Mahakama ya KImataifa ya Michezo-CAS. Uamuzi wa UEFA umekuja baada ya mkutano wa Bodi ya Vilabu ya Kudhibiti Matumizi Makubwa ya Fedha-CFCB uliofanyika jijini Nyon kuzungumzia adhabu zilizotolewa kwa vilabu nane kwa matumizi makubwa ya fedha. UEFA imesema mbali na Malaga lakini pia vilabu vya Hadjuk Split na NK Osijek za Croatia, Dynamo Bucharest ya Romania, FK Partizan na FK Vojvodina za Serbia na pia zimeondolewa adhabu ya kufungiwa baada ya kufuata masharti waliyopewa.

No comments:

Post a Comment