Sunday, May 19, 2013

VILANOVA KUREJEA NEW YORK KWA MATIBABU YA SARATANI.

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova amebainisha kuwa anatarajia kurejea jijini New York Marekani kwa ajili ya kuendelea na tiba ya matibabu yake ya saratani ya koo. Vilanova alitumia muda wa wiki 10 nchini Marekani mapema mwaka huu kwa ajili ya tiba za mionzi lakini alirejea kuijunga na kikosi chake Aprili. Kocha huyo alipanga kwenda kupata matibabu zaidi mwishoni mwa msimu lakini yeye pamoja na viongozi wa klabu hiyo walikubaliana kuwa anaweza kwenda New York kesho lakini anategemea kurejea Barcelona kwa ajili ya mchezo dhidi ya Espanyol Jumapili ijayo. Katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha kuondoka kwa Vilanova kwa kipindi cha wiki moja lakini atarejea Jumapili ijayo kwa ajili ya mchezo dhidi ya Espanyol.

No comments:

Post a Comment