Sunday, June 2, 2013
BAYERN YAFANIKIWA KUSHINDA MATAJI MATATU MFULULIZO.
WINGA machachari wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery ameonyesha furaha yake baada ya klabu yake kuifunga Stuttgart kwa mabao 3-2 katika fainali ya DFB-Pokal na kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza nchini Ujerumani kushinda mataji matatu kwa mkupuo. Bayern walifanikiwa kuweka kibindoni taji la Ligi Kuu ya Ujerumani mapema mwezi uliopita kabla ya kufanikiwa kuwafunga mahasimu wao Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali ya kufanikiwa kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema kuwa anajisikia furaha na mafanikio hayo ya kihistoria waliyopata ni kutokana na juhudi pamoja na malengo waliyojiwekea. Ribery aliwashukuru wachezaji wenzake pamoja na mashabiki ambao wamekuwa nao katika kipindi chote na kuahidi kuwa ataendelea kuwepo klabuni hapo kwa kipindi kirefu kijacho. Naye nahodha wa klabu hiyo Philipp Lahm aliongeza kuwa juhudi zao za ndani na nje ya uwanja ndizo zilizowafikisha hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment