Sunday, June 16, 2013

BRAZIL YAANZA VYEMA MICHUANO YA SHIRIKISHO.

Baada ya miezi kadhaa ya hofu kubwa kutokana na kucheleweshwa kwa maandalizi, hatimaye michuano ya Kombe la Shirikisho imeanza na mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji timu ya taifa ya Brazil na Japan mchezo ambao ulipigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Brasilia. Katika mchezo huo Brazil ilishinda kirahisi kwa mabao 3-0 ambayo yalifungwa na Neymar katika dakika ya tatu ya mchezo, Paulino dakika ya 48 na Jo aliyehitimisha karamu hiyo ya magoli katika dakika za mwisho. Michuano hiyo ya wiki mbili inapigwa katika miji sita ambayo ni Brasilia, Belo Horizonte, Fortaleza, Recife, Rio de Janeiro na Salvador huku ikitarajiwa kuvutia watu zaidi 355,000 wa Brazil na watalii kutoka nje. Michuano hiyo inaendelea tena leo kati ya Mexico na Italia ikifuatiwa na michezo kati ya Hispania na Uruguay pamoja na Tahiti na Nigeria hapo kesho.

No comments:

Post a Comment