Sunday, June 2, 2013

DJOKOVIC AFIWA NA KOCHA WAKEWA ZAMANI.

MCHEZAJI tenisi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kumchakaza mchezaji anayechipukia Grigor Dimitrov. Djokovic alifanikiwa kumfunga Dimitrov kwa 6-2 6-2 6-3 kabla ya kupewa taarifa mbaya za kifo cha kocha wake wa zamani Jelena Gencic ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 77. Gencic ambaye amewahi pia kufanya kazi na Monica Seles na Gora Ivanisevic, ndio alikuwa kocha wa kwanza wa Djokovic akiwa na miaka sita ambapo alimfundika kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa kuonyesha jinsi gani alivyoguswa na msiba huo Djokovic alishindwa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa jana ambapo anatarajia kurejea uwanjani tena Jumatatu kukwaana na Philipp Kohlschreiber wa Ujerumani.

No comments:

Post a Comment