Sunday, June 16, 2013
HAKUNA ANAYETUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU CONFEDERATION CUP.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa hawajapata chochote katika vipimo vyote walivyofanya kwa ajili ya kubaini wachezaji wanaotumia dawa za kuongeza. Hatua hiyo imekuja baada ya kumpima kila mchezaji katika kila nchi nane zinazoshiriki michuano hiyo ambayo imeanza kutimua vumbi jana. Ofisa mkuu wa masuala ya afya wa FIFA Jiri Dvorak amesema hakuna mchezaji yoyote aliyekutwa na vimelea vya madawa yaliyokatazwa michezoni baada ya kuchukuliwa vipimo vya mkojo na damu vilivyofanyika katika maabara ya Lausanne, Switzerland. FIFA imekuwa ikijipanga vyema kuhakikisha inakomesha suala la wachezaji wadanganyifu wanaotumia dawa za kuongeza nguvu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment