Saturday, June 1, 2013

MADRID YAFIKIRIA KUUZA HAKI ZA JINA LA UWANJA WAKE.

KLABU ya Real Madrid inafikiria kuuza haki za jina la uwanja wake wa Santiago Bernabeu ikiwa ni sehemu ya kutafuta njia mpya za kujiongezea mapato. Alhamisi iliyopita klabu hiyo ilitangaza kuwa kampuni ya Emirates ndio watakaochukua nafasi ya Bwin wakiwa kama wadhamini wapya wa fulana zao kuanzia msimu ujao katika mkataba ambao una thamani ya euro milioni 125 kwa kipindi cha miaka mitano. Rais wa Madrid Florentino Perez amesema wanataka kutengeneza timu iliyo imara na sehemu ya hilo itakuja kupitia ushirikiano na makampuni makubwa na kwasasa wana ushirikiano na kampuni hiyo kubwa ya ndege duniani. Rais huyo aliendelea kusema kuwa uwekezaji wa kifedha hauwezi kuishia hapo kwani klabu hiyo sasa inaangalia mwekezaji mwingine ambaye atafaa kwa ajili ya uwanja wao wa Santiago Bernabeu. Kama suala hilo likifanikiwa Madrid itakuwa imeungana na vilabu vingine ambavyo viwanja vyao vinatumia majina ya wadhamini kama Bayern Munich wanaotumia Uwanja wa Allianz Arena, Borussia Dortmund wanaotumia Uwanja wa Signal Iduna Park, Manchester City wanaotumia uwanja wa Etihad na Arsenal wanatumia uwanja wa Emirates.

No comments:

Post a Comment