Monday, June 10, 2013

WAANDAMANAJI WAOPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA UFARANSA, WAVAMIA FAINALI YA TENISI.

MCHEZA tenisi nyota wa Hispania, Rafael Nadal amefanikiwa kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kunyakuwa mataji nane ya michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kumfunga David Ferrer katika mchezo wa fainali iliyofanyika jijini Paris. Katika mchezo huo uliofanyika jana, ilibidi usimamishwe kwa muda kidogo baada ya waandamanaji wanaopinga ndoa za jinsia moja nchini humo kuvamia uwanjani kabla ya kudhibitiwa na watu usalama na kutolewa nje. Lakini pamoja na tukio hilo Nadal aliendelea kumnyanyasa mpinzani wake na kufanikiwa kushinda kwa seti zote tatu zenye alama za 6-3 6-2 6-3. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo mara baada ya kumalizika kwa mchezo Nadal amesema alishitushwa kwa muda kwasasa muandamanaji huyo alitokea kwa nyuma yake lakini baadae alitulia baada ya kugundua kuwa ni mojawapo ya watu ambao kuwazuia huwa ni ngumu. Nadal pia aliwashukuru watu wa usalama waliokuwepo uwanjani hapo na kudai kuwa walifanya kazi kubwa kuhakikisha usalama unarejea na mchezo unaoendelea.

No comments:

Post a Comment