Friday, July 19, 2013

ARSENAL YAZIDI KUMKOMALIA SUAREZ.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ameruhusiwa kuongeza ofa kufikia paundi milioni 40 kwa ajili ya kuiwinda saini ya mshambuliaji nyota wa Liverpool Luis Suarez. Mshambulijai huyo wa kimataifa wa Uruguay ndiye mchezaji anayepewa kipaumbele kusajiliwa na Arsenal msimu huu wa majira ya kiangazi ambapo tayari ofa yao ya kwanza ya paundi milioni 30 ilikataliwa na klabu hiyo. Mapema wiki hii kulikuwa na tetesi kuwa Arsenal walianzisha mazungumzo na maofisa wa Liverpool kwa kutoa ofa ya paundi milioni 35 lakini nayo ilikataliwa na kuweka wazi kuwa kiasi hicho hakikutosha. Lakini ofa mpya ya paundi milioni 40 inatarajiwa kutikisa mkataba wa Suarez huku wakala wake akidai kuwa ofa hiyo inashawishi hivyo Liverpool wanatakiwa kuisikiliza.

No comments:

Post a Comment