Sunday, July 21, 2013
BINGWA WA ZAMANI WA OLIMPIKI ATAKA ADHABU YA WANARIADHA WADANGANYIFU KUONGEZWA MPAKA KUFIKIA MIAKA MINNE.
MWENYEKITI wa michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka jana, Sebastian Coe amedai kuwa adhabu ya kufungiwa wanariadha wanaogundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu iongezwe kutoka miaka miwili hadi miaka minne. Kauli ya Coe ambaye amewahi kushinda medali mbili za dhahabu katika michuano olimpiki, imekuja baada ya wanariadha nyota wa mbio fupi Tyson Gay wa Marekani na Asafa Powell kugundulika kutumia dawa hizo katika vipimo walivyofanyiwa. Coe amesema hatua za haraka na makusudi za kuongeza adhabu hiyo kutoka miaka miwili mpaka miaka minne inabidi zichukuliwe ili kulinda heshima wa mchezo huo. Coe ambaye aliwahi kunyakuwa medali za dhahabu katika michuano ya riadha ya olimpiki mita 1,500 jijini Moscow mwaka 1980 na Los Angeles mwaka 1984 amedai kuwa bila kuchukua hatua kama hizo mchezo wa riadha utapoteza umaarufu wake kutoka na udanganyifu unafanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment