Sunday, July 21, 2013

JINAMIZI LA MAJERUHI LAANZA KUIANDAMA ARSENAL.

KLABU ya Arsenal imeendelea kuongeza majeruhi katika ukuta wake baada ya Laurent Koscilny kutolewa mazoezini kutokana na kuumia. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitolewa dakika za mwisho za mazoezi ya klabu hiyo huku akichechemea kutokana na maumivu kifundo cha mguu wake wa kulia. Baada ya beki huyo kuumia mara alifanyiwa uchunguzi na timu madaktari wa klabu hiyo kabla ya kuhamishwa na kupelekwa ndani katika Uwanja wa Rugby wa Mizuho kwa uchuzi zaidi. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kuumia katika kikosi cha Arsene Wenger toka watue nchini Japan kwa ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya ambapo golikipa Wojciech Szczesny naye aliondolewa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nagoya utakaopigwa Jumatatu usiku baada ya naye kuumia mazoezini.

No comments:

Post a Comment