Monday, July 22, 2013

MESSI AMPIGIA CHAPUO MARTINO KUCHUKUA MIKOBA YA VILANOVA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amempigia chapuo kocha Gerardo Martino kuchukua nafasi ya kuinoa klabu hiyo. Nafasi imekuwa wazi kufuatia aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tito Vilanova kulazimika kuachia ngazi kutokana na maradhi ya saratani yanayomsumbua. 
Martino ambaye aliiongoza timu ya Old Boys kushinda taji la Ligi Kuu chini Argentina msimu uliopita ni mmoja wa makocha wanaoewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Vilanova na Messi ana imani kuwa kocha huyo anastahili nafasi hiyo. Messi alidai kuwa Martino ni mmoja wa makocha wenye kiwango cha juu na kila mtu anamheshimu hivyo haoni tatizo kama akikabidhiwa mikoba ya kuinoa Barcelona.

No comments:

Post a Comment