
Thursday, July 18, 2013
POWELL AKIMBIWA NA MDHAMINI KWA KASHFA YA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.
KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Li-Ning ya China nayo imefuata nyayo za kampuni ya Adidas kwa kusimamisha udhamini kwa mwanariadha nyota wa mbio fupi Asafa Powell wa Jamaica baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli. Mapema wiki hii Adidas ambao ndio walikuwa wadhamini wa mwanariadha nyota wa Marekani Tyson Gay walisimamisha udhamini kutokana na sababu kama hizo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni hiyo iliyotumwa katika mtandao, imedai kuwa wanaheshimu mchango na kazi ngumu ya mwanariadha huyo lakini hawana jinsi bali kusimamisha udhamini wao kwake mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika. Taarifa ya Li-Ning iliendelea kudai kuwa watavunja mkataba na mwanariadha huyo bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 kama atakutwa na hatia ya kutumia dawa hizo zilizokatazwa michezoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment