MCHEZAJI tenisi nyota kutoka Serbia Novak Djokovic amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Rogers inayofanyika Montreal kwa kumgaragaza Richard Gasquet wa Ufaransa kwa 6-2 6-4. Djokovic anayeshika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani alimfunga Gasquet anayeshika namba tisa kwa kutumia dakika 52 pekee ambapo atakutana na Rafael Nadal wa Hispania katika hatua hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Djokovic mwenye umri wa miaka 26 amesema amefurahishwa na ushindi aliopata na anatemegea kufanya vyema katika mchezo unaofuata ingawa amekiri utakuwa mgumu kutokana na minzani anayekutana naye. Kwa upande wa Nadal ambaye anashika nafasi ya nne katika orodha za ubora amekiri kuwa uwanja mgumu wanaotumia unampa nafasi Djokovic ya kutinga fainali lakini hataweza kumuachia kirahisi.

No comments:
Post a Comment