KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona amedai kuwa hana mpango wa kuondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi pamoja na klabu ya Machester United kuonyesha nia ya dhati ya kumuhitaji. United ilishuhudia ofa zake mbili zikikataliwa na Barcelona huku mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Andoni Zubizarreta akiitaka timu hiyo kumsahau Fabregas kwa kipindi hiki. Kauli ya Fabregas aliyoitoa jana kuwa hana mpango wa kuondoka Barcelona na kwamba anafurahia kuwepo hao itakuwa mwiba mchungu kwa United ambao walikuwa wakijipanga kuongeza ofa ya tatu kwa ajili ya nyota huyo mwenye miaka 26. Fabregas alifafanua kuwa ni heshima kubwa kwake klabu kama United kuhitaji huduma yake lakini akadai kuwa hakuna mazungumzo aliyofanya na klabu yoyote toka ajiunge na Barcelona akitoea klabu ya Arsenal mwaka 2011.

No comments:
Post a Comment