KATIKA harakati za kupunguza vurugu katika soka nchini Argentina, msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo utaanza mwishoni mwa wiki hii kwa wanachama pekee kuruhusiwa kuingia viwanjani na kutizama mechi zao za nyumbani. Sheria hiyo itaendelea kwa wiki mbili za kwanza na baada ya hapo hatua itakayofuata ni kuwazuia mashabiki wa pinzani kuhudhuria mechi. Katika kipindi cha karibuni soka nchini humo limekuwa likimbwa na vurugu za mara kwa mara ambapo mwezi uliopita mashabiki wawili wa klabu ya Boca Juniors waliuawa katika majibishano ya risasi kati ya makundi ya wahuni ambao hishabikia klabu hiyo. Tahadhari hiyo imechukuliwa baada ya Chama cha Soka nchini humo kulaumiwa kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti vurugu hizo ambazo zinaonekana kuota mizizi.
No comments:
Post a Comment