MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kuwa alimuita mshambuliaji nyota wa zamani wa Brazil Ronaldo kwa yeye ndio wa ukweli kwasababu alikuwepo kabla ya nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Kauli hiyo ya Mourinho aliitoa wiki iliyopita wakati alipomwita Ronaldo wa sasa kwamba sio wa ukweli ingawa hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alikataa kusema lolote kuhusiana na kauli hiyo ya kocha wake wake wa zamani. Hata hivyo Mourinho alitetea kauli yake hiyo aliyotoa kwa kudai kuwa alikuwa akimaanisha umri wa wachezaji hao wawili na sio ubora wao kama wengi walivyotafsiri. Mourinho jana alijikuta akiangukia pua jijini Miami ambapo Madrid ambayo kwasasa inanolewa na Carlo Ancelotti waliifunga Chelsea kwa mabao 3-1 huku mabao mawili ya Madrid yakifungwa na Ronaldo.

No comments:
Post a Comment