Friday, August 2, 2013

RAIS WA ZAMANI WA SHIRIKISHO LA SOKA LA BENIN ATUPWA LUPANGO.

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Benin, Anjorin Moucharafou amekamatwa tena na kutupwa lupango ikiwa ni siku mbili baada ya kukataa kugombea nafasi hiyo kwa muhula wa tatu. Moucharafou ambaye alifikishwa mbele ya Mahakama Julai 2011 kwa matumizi mabaya ya fedha za shirikisho hilo na kuwekwa rumande katika gereza moja la kiraia, aliitwa tena mahakamani wiki hii pamoja na mhasibu wake Cecile Houssou kwa tuhuma hizohizo za ubadhilifu. Kiongozi huyo ambaye pia ni mfanyabiashara anatuhumiwa kusifuja isivyotakiwa kiasi cha dola 650,000 za udhamini kutoka kampuni ya simu ya MTN kati ya mwaka 2008 na 2010. Mbali na kushikilia wadhifa huo nchini kwao lakini pia Moucharafou amewahi kuwa mjumbe katika kamati za utendaji za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.

No comments:

Post a Comment