MMILIKI wa klabu ya Liverpool, John Henry amedai kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Luis Suarez hatauzwa katika kipindi hiki cha uasajili wa majira ya kiangazi na kuwa itakuwa ni kama kejeli kumruhusu kujiunga na mahasimu wao klabu ya Arsenal. Wakati Suarez mwenyewe akitangaza hadharani nia yake yake ya kuondoka Anfield ili aweze kupata nafasi ya kucheza katika klabu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa, Henry kwa upande wake amemua kumuwekea ngumu mchezaji huyo. Arsenal tayari walishatoa ofa ya paundi milioni 40 kwa ajili ya Suarez lakini Henry amedai kuwa ni suala lisilozungumzika kumuuza mchezaji wao bora kwa klabu ambayo nayo inatafuta nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa. Henry amedai kuwa anadhani Suarez bado anaweza kushawishiwa kubaki Liverpool kwa ajili ya msimu ujao na utata huo hauwezi kuwazuia kufanya vizuri huko mbele.

No comments:
Post a Comment