Wednesday, September 4, 2013

MULLER AIPONDA MADRID KUMRUHUSU OZIL KWENDA ARSENAL.

NYOTA wa kimataifa wa Ujerumani, Thomas Muller amekuwa mchezaji wa kwanza kuponda hatua ya klabu ya Real Madrid kumruhusu Mesut Ozil kujiunga na klabu ya Arsenal. Madrid walitia kibindoni kitita cha euro milioni 50 kwa kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye walimnunua kutoka klabu ya Werder Bremen kwa ada ya euro milioni 15 mwaka 2010. Muller amekiri kuwa haelewi kwanini Madrid waliamua kumuuza mchezaji huyo ambaye alipendwa na wachezaji wenzake pamoja na mashabiki. Muller aliendelea kudai kuwa kwa usajili waliofanya Madrid msimu huu hawakupaswa kumruhusu Ozil kuondoka lakini muda mwingine mambo kama hayo hutokea katika soka. Kwa upande wake Muller amesema hana mpango wowote wa kuikacha klabu yake ya Bayern na kukiri kuwa na furaha kufanya kazi chini kocha mpya Pep Guardiola kama ilivyo kwa Joachim Loew katika timu ya taifa ya Ujerumani.

No comments:

Post a Comment