MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo anaweza kuwa ameweka saini na kuwa mchezaji analipwa zaidi katika ulimwengu wa soka kwa kukunja kitita cha paundi 288,000 kwa wiki lakini nyota huyo sio pekee mwenye mafanikio katika familia yao. Dada yake Ronaldo ambaye ni muimbaji aitwae Katia Aveiro anatarajia kuachia kibao chake matata Septemba 18 mwaka huu kinachokwenda kwa jina la Boom Sem Parar kwa lugha ya Kihispania ambayo inamaanisha Nonstop Boom kwa kiingereza.
Hii itakuwa rekodi yake ya kwanza kuitoa kimataifa baada kufanya vizuri katika vibao vyake kadhaa nchini Hispania na Ureno na kuingia mkataba na waandaji wa muziki wanaofahamika duniani. Akihojiwa kuhusiana na ujio wake huo mpya mwanadada huyo aliyeweka maskani yake jijini Madrid amesema ni heshima kubwa kwake kuweza kufanya kazi na waandaaji hao maarufu na wenye vipaji na ana mategemeo mashabiki na vyombo vya habari duniani kote wataipokea vizuri singo yake hiyo. Mwanadada huyo mwenye mvuto kama ilivyo kwa kaka yake aliongeza kuwa huo ni mwanzo tu wa safari yake ndefu ya kimuziki kimataifa.
No comments:
Post a Comment