Wednesday, October 16, 2013

IT'S NOT OVER YET - APPIAH.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah, amewataka wachezaji wake kutobweteka kutokana na ushindi mnono wa mabao 6-1 waliopata dhidi ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia hatua ya mtoano. Appiah amesema kwasasa hawapaswi kushangilia kwanza kwasababu bado dakika nyingine 90 ili waweze kuwa na uhakika wa kwenda Brazil mwakani. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kitu cha muhimu hivi sasa ni kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili kwani misri nao hawataifanya kazi yao iwe rahisi pamoja na kupoteza mchezo kwa idadi kubwa ya mabao. Mechi ya mkondo wa pili baina ya timu hizo inatarajiwa kuchezwa Novemba 19 jijini Cairo.

No comments:

Post a Comment