IKIWA kampeni za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 ikifikia katika hatua tete, timu kadhaa wiki hii zinatarajia kukata tiketi kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa kabisa duniani. Wenyeji Brazil tayari wameungana na nchi za Japan, Australia, Iran na Korea Kusini kwa upande wa bara la Asia huku Ulaya kukiwa tayari na nchi za Uholanzi, Italia, Ujerumani, Ubelgiji na Switzerland wakati Concacaf kuna timu za Marekani, Costa Rica pamoja na wenzao wa Amerika Kusini Argentina na Colombia. Wiki hii nchi nyingine kutoka bara la Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini na Kusini zinaweza pia kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo. Kwa upande wa Ulaya, Urusi inaweza kujikatia tiketi kama wakifanikiwa kuwafunga Azerbaijan huku Ugiriki nao wakiwa na nafasi kama hiyo kama wakifanikiwa kuwafunga Bosnia-Herzegovina wakati Uingereza na mabingwa watetezi wa michuano hiyo nao wakiwa wamebakisha hatua moja kufikia huko. Kwa upande wa Afrika mechi za hatua ya mtoano zitaendelea kesho ambapo Ivory Coast na Nigeria zitajitupa uwanjani kutetea ushindi wa mechi za mkondo wa kwanza wakati Tunisia itasafiri kuifuata Cameroon Alhamisi baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana mwishoni mwa wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment