Monday, October 21, 2013

ORLANDO PIRATES, AL AHLY KUKWAANA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.

KLABU ya Al Ahly ya Misri imejiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuifunga Coton Sport ya Cameroon kwa changamoto ya mikwaju ya penati na kutinga fainali. Al Ahly walishinda kwa matuta 7-6 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika nusu fainali ya mkondo wa pili iliyofanyika huko El-Gouna. Katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza timu hizo pia zilitoka sare ya bao 1-1 hivyo kufanya timu hizo hizo kufungana jumla ya mabao 2-2 katika mechi mbili walizokutana. Al Ahly sasa watakwaana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika fainali ya mikondo miwili itakayochezwa mwezi ujao.


No comments:

Post a Comment