Tuesday, December 3, 2013

MESSI, RONALDO WAGAWANA TUZO HISPANIA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga katika msimu wa 2012-2013 huku nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akipigiwa kura kama mchezaji mwenye thamani zaidi. Nyota huyo wa Barcelona ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya tano mfululizo na pia kuchukua zawadi ya mshambuliaji bora, wakati mchezaji mwenzake Andres Iniesta kama mmoja wa viungo bora kwa mara ya nne kwa misimu mitano. Akipokea zawadi hiyo Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 alishukuru wachezaji wenzake wa Madrid kwani bila wao kumsaidia asingeweza kupata zawadi hiyo. Tuzo hizo zimekuja ikiwa zimebaki siku zoezi la upigaji kura kusitishwa kwa ajili ya kuchagua mchezaji bora wa mwaka wa dunia ambapo Ronaldo na Franck Ribery ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo.


No comments:

Post a Comment