Wednesday, December 4, 2013

VIWANJA VITATU VYA KOMBE LA DUNIA KUSHINDWA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa viwanja vitatu vinavyojengwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil vitavuka muda uliopangwa katika kukamilika kwake. Viwanja hivyo ambavyo ni Arena Pantanal kilichopo katika mji wa Cuiaba, Arena da Baixada uliopo Curitiba na Arena Corinthians uliopo jijini Sao Paulo ndivyo vinavyotarajiwa kuvuka muda wa mwisho ambao ni Desemba 31 mwaka huu. Rais wa FIFA, Sepp Blatter alitoa rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika ajali iliyoua watu wawili katika Uwanja wa Corinthians mwezi uliopita lakini akadai kuwa uwanja huo utakuwa tayari kwa ajili ya mechi ya ufunguzi itakayochezwa Juni 12 mwakani. Blatter aliongeza kuwa tatizo la viwanja hivyo kutokamilika kwa wakati ni dogo hivyo wanaweza kulifumbia macho. Blatter amesema viwanja vyote hivyo na vingine vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo vitakuwa vimekamilika ifikapo Februari mwakani.


No comments:

Post a Comment