Thursday, January 9, 2014
BAADA YA KURUDI KWA NGUVU ZOTE MESSI ADAI ATAZEEKEA BARCELONA.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amedai kuwa anataka kumalizia soka lake katika timu hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza toka arejee uwanjani kutokana na majeraha. Mabao hayo mawili aliyofunga nyota huyo yameiwezesha timu hiyo kuifunga mabao 4-0 Getafe katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Mfalme uliofanyika jana. Kauli hiyo ya Messi imekuja kufuatia tetesi kuwa klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa inajiandaa kutoa ofa kabambe kwa ajili ya kumnasa baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na mkurugenzi wa timu hiyo Javier Faus. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi alikanusha uvumi na kudai kuwa anataka kubakia Camp Nou mpaka atakapostaafu kucheza soka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment