BEKI mahiri wa klabu ya Bayern Munich, Dante anaamini kuwa Manuel Neuer ndio golikipa bora duniani kufuatia kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2013-2014. Golikipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani alitajwa kama golikipa bora duniani na Shirikisho la Kimataifa la Historian a Takwimu za Soka-IFFHS mapema mwaka huu na Dante anafikiri mchezaji mwenzake huyo alistahili tuzo hiyo. Akihojiwa Dent mwenye umri wa miaka 30 amesema siku zote wanakuwa na madhumuni ya kumlinda golikipa wao ili wasimuweke katika nafasi ngumu lakini huwa wanajiamini zaidi kwa kujua kuwa wana golikipa bora duniani nyuma yao. Neuer amefanikiwa kuzuia nyavu zake kutikiswa katika mechi 16 za Bundesliga msimu huu.

No comments:
Post a Comment