Wednesday, February 5, 2014

BOSI WA BAYERN AITAKA UEFA KUIADHIBU PSG KWA MATUMIZI HOLELA YA FEDHA.

MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amelitaka Shirikisho la Soka barani ULaya, UEFA kuchukua hatua dhidi ya klabu ya Paris Sain-Germain kama walivunja sheria mpya ya matumizi ya fedha ambayo inatarajiwa kuanza kufanya kazi Julai mosi mwaka huu. Rummenigge katika kipindi cha karibuni amekuwa na wasiwasi kuhusu matumizi ya PSG na sasa amemtaka rais wa UEFA Michel Platini kutoa adhabu kwa maibingwa hao wa Ufaransa kama watakuwa wamekiuka taratibu. Bosi huyo wa Bayern aliendelea kudai kuwa ni jambo gumu kufikiria kuwa PSG wanafuata sheria hiyo mpya ya matumizi ya fedha haswa ikizingatiwa fedha nyingo zinazoingia kutoka Qatar. Hivyo ameitaka UEFA kuhakikisha inaisimamia sheria hiyo baada ya vilabu kupewa kipindi cha miaka mitatu ili kufikia vigezo wanavyovitaka kuhusiana na masuala ya matumizi.

No comments:

Post a Comment